......................................................................
Na Esther Macha, Mbeya
Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya Serikali
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya vyandarua hali hiyo bado
imekuwa tatizo kutokana jamii zilizo nyingi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya
kuwa na imani potofu kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa kuwa hawapati
usingizi na wengine kudai ni njia ya uzazi wa mpango.
Hayo yalisemwa jana
Bwana afya katika Ofisi ya Wilaya ya Mbarali Bw.Yona Msyani wakati wa mahojiano
maalumu na gazeti hili, kuhusiana na elimu ya ugonjwa wa maralia katika
viwanja vya hospitali ya Chimala Mission .
Alisema kuwa suala la
utumiaji wa vyandarua imekuwa changamoto kubwa kwa katuiika utendaji kazi kwa
wataalamu wa afya kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu ya matumizi
ya vyandarua vyenye dawa.
“Bado tuna changamoto kubwa sana hivyo inatupasa kujipanga na kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa matumizi ya vyandarua “alisema.
Hata hivyo alisema kuwa imani hiyo potofu si kwa Wilaya ya mbarali tu kwani hali hiyo ilijitokeza wakati wa kampani ya ugawaji wa vyandarua hivyo mwaka 2010 kwa nchi nzima.
Akizungumzia kuhusu vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa maralia ,Bwana afya huyo alisema kuwa maralia I ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Tatizo hili lipo kwa kiasi kikubwa kwa watoto , mwaka 2012 mwezi januari mpaka desemba waliugua watoto 1,635 chini ya umri wa miaka mitano ambapo kati ya hao waliofariki ni 100 kwa mwaka jana kutokana na ugonjwa wa maralia.