Nimeamshwa
na simu kutoka Emergency Alert ya mji wa Cambridge , MA wakisema kuwa
ni maarufu kutoka nje ya majumba yetu leo! Hakuna usafiri, wameomba
sehemu za kazi zisifungue!
Wanasema kuwa hakuna kufungua mlango hata kama ni polisi, wanasema kuwa jamaa anataka kuua watu!
Jana
usiku ilikuwa balaa hapa Cambridge! Cambridge ni nje ya Boston. Kwanza
kwenye saa tatu na nusu (9:30PM) tulisikia kuwa majambazi walivamia
duka la 7-11 Central Square!
Kukaa kidogo tukasikia Polisi kapigwa risasi Chuo Kikuu cha MIT! Baada ya muda mfupi wakasema yule polisi kafa!
Kwenye
saa tano tukasikia mtu kaibiwa gari yake aina ya Mercedes Benz, kwenye
kituo cha mafuta! Ni mwendo mfupi toka ninapokaa! Nikaanza kusikia
milio ya gari ya polisi!
Kumbe polisi wa kila aina walikuwa wanawafukuza karibu na Arsenal Mall. Milio ya risasi balaa, ambulance na
magari ya polisi yalikuwa yanafukuzana, kwenye TV, tukaona kila mtu
aliyefanana na Mspanish, Mwarabu kasimamishwa na kusachiwa!
Sikulala hadi saa nane na nusu! Nimeamshwa na simu ya Emergeny Alert!
Duh, hii ni kama SINEMA!
Wanasema
huyo gaidi wanayetamfuta anaitwa Zohkar Sarnev mwenye miaka 19,
anatoka Chechnya! Huyo gaidi wanayemtafuta, nilikuwa nawaona hapa
Cambridge lakini nilidhani ni wanafunzi wa kawaida!