Mikutano
ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013
na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Kila kunapokuwa na
mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa
habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta
za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya
kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la kimataifa pamoja na
kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia
na Shirika la Fedha la Kimataifa.
PICHANI JUU: Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
Wajumbe
wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo
pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa
BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar
Bi. Bihindi Nassor pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe
kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa
mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
...Kikao kikiendelea...
Kutoka
kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa
Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa
makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya
Fedha Bw. Patric Pima.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh
wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu
masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw.
Paul Mwafongo.