Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, June 3, 2013

KONGAMANO LA WAISILAMU JIJINI DAR, .... JIONEE MAMBO YALIVYOKUWA ....

Waumini wa dini ya Kiisilamu wakiwa kwenye Kongamano lililofanyika leo jijini Dar es Saalaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na masheikh. Msimamo wa waisilamu juu ya Maendeleo ya mchakato wa katiba mpya, Dhulma na uonevu dhidi ya waisilamu pamoja na hatua za kuchukuwa kama madai yao yatapuuzwa.                 
Hivi ndivyo Diamod ilivyofurika.
Waisilamu wa Rika na jinsi zote walikuwepo.
Imamu wa Msikiti wa Mtambani Imam Suleiman akimkaribisha Sheikh Ponda kuhutubia waisilamu kwenye Kongamano hilo.
Takibirrrrr zikafuatia baada ya kukaribishwa Sheikh Ponda.
Sheikh Konda Juma Bungo nae aliwasilisha mada.
Sheikh Ponda Issa Ponda  (kushoto) akihutubia waisilamu kwenye kongamano hilo.
Sheikh Ally Basaleh nae hakusita kuwaambia serikali kuwa kwenye daladala waliopanda watanzania kuna watu wamevaa ndala na kuna wengine wamevaa buti wenye ndala wanakanyagwa ndio maana wanasema! Kwahiyo badala ya kufanya hasira na kuchukua maamuzi ya nguvu bora wawasikilize wanaosema wanakanyagwa.
Amiri wa Jumuia na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Musa Kundecha nae aliwaambia waisilamu kuwa kwa kawaida mtu akilala ukimwamsha huamka lakini ukimwona amelala una mwamsha na haamki basi ujue hajalala ila anajifanya amelala dawayake ni kumkera mpaka aamke.
Jopo la Masheikh wa Meza kuu.

Na Mwandishi Maalum.
WAISILAM leo wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania jijini Dar es Salaam.
Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya katiba mpya ambapo walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.
Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka tuamini kwamba anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabra hata wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waisilamu wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapimziko kwa miaka nenda rudi hawapewi wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“W aisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua.
Aidha heikh Ponda alifafanua kuwa waisilamu wavumilie wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na mchana mpaka kieleweke nchi nzima.
Sheikh Ally Basaleh alisihi Serikali kuwasikiliza waisilamu hoja zao wasiwapuuze.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...